Jumanne 20 Januari 2026 - 18:00
Mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni na Marekani yataendelea kwa umakini na nguvu zaidi

Hawza/ Mshauri wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi katika masuala ya kimataifa, akirejea mwenendo wa hivi karibuni nchini Iran, alisema: Kwa fadhila ya msaada wa Mwenyezi Mungu, njama hii ilidhoofishwa na kufeli, lakini mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni na Marekani yataendelea kwa umakini na azma kubwa zaidi.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Dk. Ali-Akbar Welaayati', Mshauri wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi katika masuala ya kimataifa, kwenye mazungumzo ya simu na Nouri al-Maliki, mmoja wa wanachama wa “Mfumo wa Uratibu” unaojumuisha vyama vya Kishia vya Iraq, walibadilishana mawazo kuhusu maendeleo muhimu zaidi ya kikanda na kimataifa, ikiwemo mahusiano kati ya Iraq na Iran.

Dk. Wilayati katika mazungumzo haya aliupongeza ushindi wa taifa kubwa la Iraq katika uchaguzi wa hivi karibuni wa wabunge na ushiriki wao mkubwa na wa shauku, na akaongeza: Ushindi huu, ambao ulipatikana chini ya usimamizi na uongozi wa watu wakubwa kama wewe, umeimarisha msimamo wa Iraq katika eneo na ulimwenguni kwa ujumla.

Akiendelea kuwa, kwa kurejea mwenendo ya hivi karibuni nchini Iran, alimwambia Maliki: Bila shaka mnafahamu matukio ya hivi karibuni nchini Iran na misimamo iliyo wazi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi kuhusu suala hili; ambapo alieleza kuwa; kushindwa kwa Marekani mikononi mwa taifa la Iran katika tukio hili ni mwendelezo wa kushindwa kwao huko nyuma, pamoja na kushindwa kwao na kwa utawala wa Kizayuni katika vita vya siku 12. Aidha alisisitiza kuwa, adui kwa maandalizi mapana, aliendesha njama hii kwa ajili ya malengo makubwa zaidi, lakini taifa la Iran liliidhoofisha na kuibatilisha. Hata hivyo, hili halitoshi, na Marekani inapaswa kuwajibika kwa matendo yake.

Akiashiria kauli za Kiongozi wa Mapinduzi, aliongeza kuwa: Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi alisema kwamba kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, taifa la Iran, kama lilivyouvunja mgongo wa fitna, linapaswa pia kuvunja mgongo wa mfitni mwenyewe.

Dk. Wilayati alisisitiza kwamba: Kwa fadhila ya msaada wa Mwenyezi Mungu, njama hii ilifeli, lakini mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni na Marekani yataendelea kwa umakini zaidi. Tukio hili halikuwa dhidi ya Iran pekee, bali ni njama dhidi ya eneo zima; na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Iran, Iraq, Hizbullah ya Lebanon, Palestina na Ansarullah ya Yemen watasimama imara mbele ya madhalimu wote, hususan Wazayuni.

Mshauri wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi katika masuala ya kimataifa pia aliunga mkono azma ya serikali na taifa la Iraq ya kuwafukuza majeshi ya Marekani na NATO kutoka Iraq na kukomesha uvamizi wa nchi hiyo unaofanywa na majeshi hayo. Aidha, alisema kulinda umoja wa ardhi ya Iraq, ustawi na maendeleo ya watu wake kuwa ni miongoni mwa vipaumbele muhimu vya kikanda vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kwa upande wake, Nouri al-Maliki katika kujibu, huku akionesha shukran zake kutokana na maoni ya Dk. Wilayati, alisema: Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, hakutabakia machafuko wala njama yoyote, si Iraq wala Iran; kwa sababu tukio lolote nchini Iran lina athari ya moja kwa moja kwa Iraq na eneo zima.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha